Sera ya Faragha
1 Utangulizi
Karibu kwenye NEKEZA. Tunathamini faragha yako. Sera hii inaeleza jinsi tunavyokusanya, kutumia, kuhifadhi, na kulinda taarifa zako unapotumia huduma zetu za mauzo, stock, usimamizi wa wafanyakazi, na customer care.
2 Data tunayokusanya
Tunaweza kukusanya aina zifuatazo za data:
- Akaunti: username, jina, namba ya simu, na taarifa za kuingia.
- Biashara: rekodi za mauzo, stock, bei, na ripoti.
- Timu: taarifa za wafanyakazi na ruhusa zao.
- Msaada: ujumbe wa customer care, tickets, na chat.
- Kifaa: data ya push notifications (ukiidhinisha).
3 Jinsi tunavyotumia data
- Kuendesha na kuboresha huduma za mauzo na stock.
- Kusimamia akaunti, muda wa matumizi, na usalama.
- Kutoa msaada kupitia Customer Care na live chat.
- Kutuma taarifa muhimu (mauzo, bidhaa, muda wa akaunti) ukiruhusu.
- Kuzuia matumizi mabaya na kulinda mfumo.
4 Uhifadhi na usalama
Data inahifadhiwa kwenye database salama (mfano Supabase / Postgres). Ufikiaji unadhibitiwa kwa majukumu (admin, boss, employee). Tunatumia hatua za kiufundi na za kiutawala kulinda data dhidi ya ufikiaji usioidhinishwa.
5 Push notifications
Ukikubali, tunaweza kutuma taarifa kwenye kifaa chako kuhusu chat, mauzo, bidhaa mpya, muda wa akaunti, au matukio muhimu ya biashara. Unaweza kuzima ruhusa kwenye settings za kifaa chako.
6 Kushiriki data
Hatouzi data yako kwa watu wa nje kwa madhumuni ya kibiashara. Tunaweza kushiriki data tu pale inapohitajika kisheria, au kwa watoa huduma wanaosaidia kuendesha app (mfano hosting / database) chini ya makubaliano ya usiri.
7 Haki zako
- Kuona na kuhariri taarifa za profile yako.
- Kuomba kufuta akaunti kupitia sehemu ya Futa Akaunti.
- Kuwasiliana nasi kuhusu maswali ya faragha kupitia Customer Care.
8 Mawasiliano
Maswali kuhusu sera hii: tumia Customer Care au Contact Admin ndani ya app. Tutajibu haraka iwezekanavyo.
Imeboreshwa: Oktoba 2026 · NEKEZA